1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani Karadzic ?

22 Julai 2008

Radovan Karadzic,mhalifu aliesakwa kwa zaidi ya muongo mmoja ametiwa nguvuni.

https://p.dw.com/p/EhU5
Wabosnia washerehekea kuamatwa Karadzic.Picha: AP

Nani Radovan Karadzic ambae baada ya kujificha miaka kadhaa sasa ametiwa nguvuni na anatakiwa na Mahkama kuu ya Kimataifa mjini The Hague,Uholanzi, akabili mashtaka hasa kwa mauaji ya waislamu hadi 8000 mjini Srebenica,hapo 1995 ?

Mtuhumiwa huyu mkubwa wa uhalifu wa vita,ni mzaliwa aliunda chama cha wazalendo cha kidemokrasi cha waserbia huko Bosnia-herzegovina hapo 1989.Mshairi na daktari kama alivyopenda kuitwa, hakukawia kuonesha ni mkondo gani wa siasa ataofuata alipokuja kuwa rais wa Serbia katika Jamhuri ya Bosnia.

1991,mfuasi huyu wa marehemu Marshall Tito, kabla uhuru wa Jamhuri ya Bosnia-Herzegovina, aliwatishia vita waislamu wa Bosnia wakati wa hotuba yake Bungeni mjini Sarajevo.

Alisema:

"Mnabidi kuelewa kuwa mtaitosa Bosnia-Herzegowina vitani -vita vitakavyo wahilikisha kabisa waislamu.Waislamu hamtaweza kujilinda pale vita vikiripuka."

Alionya Karadzic.

Nusu mwaka baada ya hotuba hii inayokumbukwa sana na baada ya kutolewa tangazo la uhuru wa Bosnia, ilikua karadzic binafsi alieitosa Bosnia-Herzegovina motoni.

Akishirikiana chanda na pete na mchochea kuni za vita -Rais wa Serbia wakati ule ,marehemu Slobodan Milosevic,Karadzic aliandaa uvamizi wa majeshi ya waserbia dhidi yavikosi vya waislamu wa Bosnia.

Karadzic na Jamadari khabithi anaendelea kusakwa aliekua mkuu wa majeshi Ratko Mladic,walieneza hofu na kihoro miongoni mwa wakaazi wa kiislamu na Croatia huko Bosnia,ingawa mbele ya wapatanishi wa kimataifa, Karadzic akidai kinyume kabisa:

Kabla ya vita, wakiishi waislamu 20,000 huko Banja Luka.Sasa wanaishi 40,000.Wamewasili kutoka vijiji vidogo ambako hatuwezi huko kuwalinda. Sasa tunawalinda hapa Banja Luka."

Alidai Karadzic mbele ya wapatanishi wa kimataifa.

Wakati akisema hayo wakaazi wa mji mkuu wa Sarajevo, uliozingirwa na majeshi yake waliweka kufa na njaa kwa miaka kadhaa.Halafu ya kafuatia mauaji ya waislamu wa Bosnia 8,000 huko Srebenica-ambayo yamegeuka alama ya mauaji ya kikatili kabisa ya kuhilikisha umma yaliotokea kati kati ya Ulaya baada ya vita vya pili vya dunia.

Kwahivyo, Karadzic na mshirika wake wa chanda na pete Vlatko Mladic ndio dhamana wa uhalifu huo.

Sasa tusubiri kusikia vipi Karadzic atajitea mbele ya Mahkama kuu ya kimataifa.Mjini Sarajevo, mji mkuu wa Bosnia tayari kutiwa kwake tu nguvuni kumesherehekewa kwa shangwe na shamra-shamra-kama kukata kiu cha muda mrefu cha madhambi makubwa waliotendewa jamaa zao.