1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NANTERRE:Waziri mkuu wa Burundi wa zamani atiwa jela Ufaransa

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOw

Waziri Mkuu wa Burundi wa zamani Gabriel Mpozagara na mkewe wamehukumiwa kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miezi 15 jela kwa kuwatumisha wapwa wao wawili kama watumwa.Bwana Mpozagara na mkewe wanatakiwa kulipa faini ya euro alfu 10 kila mmoja na kuagizwa kuwalipa watoto hao euro alfu 24 kwasababu ya mateso yaliyowasibu wakiwa mikononi mwao.Kulingana na wakili wao ,wasichana hao walitumishwa kama watumwa katika kipindi cha mwaka 94 hadi 99 nyumbani kwa mjomba wao mjini Ville d’Avray nchini Ufaransa.

Msichana mkubwa alilazimika kuhudumia jamaa zake na wana wao kwa muda wa saa 16 kwa siku kwa mujibu wa shirika linalopambana na utumwa lililowasilisha kesi hiyo mahakamani.

Wasichana hao wawili walihamia nchini Ufaransa mwaka 94 baada ya kifo cha wazazi wao katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao Burundi.Watoto hao walikuwa na umri wa miaka 9 na 13 wakati huo na baada ya miaka mitano msichana mkubwa alitoa malalamiko rasmi.