1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kuendelea kuweka kikosi Kosovo

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYkl

BRUSSELS

Mawaziri wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO leo hii wanatazamiwa kuahidi kwamba itaendelea kuweka kikosi chake cha kulinda amani huko Kosovo kama kilivyo hivi sasa wakati jimbo hilo likielekea kwenye uhuru na kupeleka vikosi zaidi itakapohitajika kukabiliana na machafuko yoyote yale ya umwagaji damu.

Viongozi wa kabila la Waalbania wa jimbo hilo la Serbia lililojitenga wanatazamiwa kujitangazia uhuru katika miezi michache ijayo baada ya kushindwa kwa usuluhishi wa kimataifa ambako kunaweza kuzusha machafuko mapya katika eneo la Balkan.

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani amesema mawaziri wa NATO watatangaza katika mkutao mjini Brussels Ubelgiji leo hii kwamba kikosi chake cha wanajeshi 16,000 cha kulinda amani kitaendelea kubakia Kosovo na uwezo wake ilionao hivi sasa.

Wasuluhishi wa kimataifa wantazamiwa kuripoti kwa Umoja wa Mataifa hapo Jumatatu kwamba juhudi za kufikia muafaka kati ya Kosovo na Serbia zimeshindwa.