1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO na hujuma za mitandaoni

12 Oktoba 2010

Wasi wasi wazidisha changamoto katika ulinzi

https://p.dw.com/p/Pcp0
Kompyuta:chombo kinachotumiwa kuingia kwenye mitandao.Picha: dpa

Shirika la kujihami la magharibi NATO linakabiliwa na changa moto kubwa zaidi kuliko ile ya ulinzi, kutokana na kuongezeka kwa kitisho cha mitandao. NATO inapanga kuzigeuza sera zake za kujilinda ikiwa ni pamoja na kuzidi kitisho hicho cha mashambulio kwa njia ya mitandao. Lakini wakati hatua za kuzilinda nchi wanachama dhidi ya virusi vya kompyuta ikiwa peke yake ni kazi ngumu, pamoja na hayo hiyo si changamoto pekee.

Kuzuka kwa virusi vya kompyuta vinavyujulikana kama Stunext ambavyo baadhi ya wataalamu wa masuala ya ulinzi wameshavitaja kuwa"silaha ya kwanza kuu katika mtandao," kumesababisha uwezekano wa kuwepo kwa vita vya mtandao na hivyo kuigeuza hali hiyo kutoka kitu cha kubuni na kuwa hali halisi inayohusika na usalama.

Mashambulio ya kirusi chenyewe:

Mdudu huyo wa ajabu katika fani ya ufundi wa elektroniki, anadaiwa kukikumba kifaa cha kiviwanda chenye ufundi wa komyputa huko nchini Iran mwezi uliopita, na kusababisha utawala wa nchi hiyo kudai ni sehemu ya shambulio la makusudi lililofanywa na mmoja au wengi miongoni mwa maadui zake dhidi ya mpango wa kinyuklia wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu. Teheran imedai kwamba Marekani na Israel mmoja wapoo au zote mbili zilikuwa nyuma ya mpango wa kuanzisha kirusi hicho.Kirusi cha Stunext ambacho huuandama mfumo wa kudhibiti mtambo fulani-mfumo uliotengenezwa na kiwanda kikubwa cha Ujerumani Siemens na ambao mara nyingi hutumika katika mifumo ya nishati, tangu wakati huo kimeripotiwa pia kuingia China ambako mamilioni ya kompyuta duniani zimeathirika.

Athari za mdudu Stunext:

Kampeni hiyo ya Stunext inadhihirisha jinsi gani kirusi hicho kinavyoweza kuingia katika Kompyuta. Katika kile kilichofikiriwa kuwa shambulio la kwanza kubwa kabisa la mfumo wa mtandao wa Kompyuta katika nchi huru , Estonia ilikumbwa na shambulio katika utaratibu wa huduma 2007 ambapo mitandao kadhaa ilijaa taarifa zisizokuwa na maana ambazo hatimae zilisababisha huduma za serikali na mabenki kufungwa. Wakati ambapo shambulio hilo lilitokea wakati wa mgogoro na Urusi kuhusiana ana kuondolewa kwa mnara wa kumbukumbu ya wakati wa vita mjini Tallin,shutuma za tukio hilo zikaelekezwa kwa Urusi.Lakini chanzo cha kirusi hicho haikuweza kugunduliwa wala kuthibitishwa. Inaaminika shambulio hilo la kiruisi katika mtandao wa Wakati kitisho cha kuhujumiwa huduma za umma pekee ni chenye kutia wasi wasi, hujuma ya virusi vya aina hiyo kwa mfumo wa ulinzi ni hali inayotia wasi wasi zaidi.

Kitisho ni kikubwa:

Kitisho hicho kinaonekana kuwa sawa na silaha mpya ya vita vipya ambapo NATO inazingatia kujumuisha neno vita vya silaha ya mtandao wa Kompyuta katika ibara ya 5 ya katiba yake inayohusiana na kulindana miongoni mwa wanachama. Pindi NATO itakubali kukiongeza kifungu hicho, Shirika hilo litakuwa na wajibu wa kujibu shambulio lolote linalotokana na mtandao wa kompyuta dhidi ya nchi yoyote mwanachama-sawa na kama taifa lolote la NATO litashambuliwa kwa silaha.NATO ambayo inauzoefu wa mashambulio madogo ya wahalifu wa Kiserbia walioingia kwenye mtandao wakati wa vita vya Kosovo 1999, inakusudia kuzungumzia kuzidi kwa kitisho cha vita vya mitandao ya kompyuta, wakati wa mkutano wake wa kilele mjini Lisbon-Ureno mwezi ujao.

Wataalamu wana shakashaka:

Hata hivyo akizungumza na Deutsche Welle,mtaalamu mmoja katika taasisi ya masuala ya usalama ya Royal United Services yenye makao yake mjini London Alex Neil, anasema, Shirika la NATO litakabiliwa na matatizo ikiwa kifungu cha kupambana na mashambulio kwa njia ya mtandao kitaingizwa katika ibara ya tano ya katiba yake. Anasema katika hatua ya kujibu shambulio lolote, kinachoweza kuonekana ni juhudi za pamoja baina ya wanachama walio na uwezo na maarifa katika fani hiyo ya mitandao, katika wakati ambapo baadhi wameendelea zaidi kuliko wengine. Hapo anaashiri kuwepo kwa hali fulani ya mgongano. Baadhi ya wanachama hawatokuwa tayari kuonyesha uwezo wao mkubwa kwa washirika wengine.

Wataalamu wanasema kujibu shambulio lolote kwa njia ya mtandao litakua jambo gumu kwa asababu ni shida , kutambua chanzo chake. Neil anasema kinachoshuhudiwa kwa sasa ni vita vya kimya kimya ambavyo havijagusa uwanja wa operesheni zenyewe. Kile kinachopigwa vita hivi sasa ni ujasusi na hujuma kwa njia ya mitandao kuliko kuwa ni vita vyenyewe ambavyo huwa ni kukabiliana ana kwa ana.

Mwandishi: Amies Nick (DW English)

Imetafsiriwa na :Mohammed Abdul-Rahman