1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaidhinisha mkakati mpya wa ulinzi

22 Novemba 2010

Merkel aipongeza Urusi kwa kushiriki mkutano wa NATO, huku Urusi nayo ikitaka fursa kamili ya kuwa mshiriki wa mikakati ya ulinzi dhidi ya makombora na sio msindikizaji tu

https://p.dw.com/p/QEXa
Katibu mkuu wa NATO Jenerali Anders Fogh Rasmussen akihutubia mkutano mjini Lisbon.Picha: AP

Katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Kujihami la NATO uliofanyika mjini Lisbon, Ureno, viongozi hao wameidhinisha mpango mpya wa miaka 10 ijayo unaoliruhusu Shirika hilo kupambana na vitisho vipya vya ugaidi.

Hii ni pamoja na uvamizi wa mitandao. Mipango ya kuunda mfumo wa pamoja wa ulinzi na Urusi, pia ilijadiliwa. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameutaja mkutano huo wa NATO kama nafasi muhimu katika uhusiano kati ya mataifa ya Mashariki na Magharibi. Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kushiriki katika mkutano huo wa NATO.

Mwandishi: Maryam Abdalla/DPAE, Reuters

Mhariri: Sekione Kitojo