1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajitenga na kauli ya Macron ya kuingiza vikosi Ukraine

Sudi Mnette
12 Machi 2024

Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg amejitenga na tamko la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba washirika wa Magharibi hawapaswi kuondoa uwezekano wa kupeleka wanajeshi Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dPSR
Deutschland | Münchener Sicherheitskonferenz | Jens Stoltenberg Generalsekretär der NATO
(Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza.Picha: Kuhlmann/MSC

Stoltenberg amesema "NATO haina mpango wa kupeleka wanajeshi Ukraine, kadhalika haina mpango kujiingiza katika mzozo huo, na wala kuhusishwa washirika wake."

Stoltenberg aliongeza, hata kama ni taifa binafsi la NATO likipeleka vikosi Ukraine hatua hiyo itaathiri  muungano huo kwa ujumla kwa kuwa wanachama wake wamefungwa na mkataba wa ulinzi wa pamoja.

Akifafanua baada ya kauli tata ya Macron, Stoltenberg amesema anadhani ni muhimu kwa kushauriana na kwamba wawe na namna ya pamoja ya kushughulikia masuala kwa sababu yana uzito kwa wanachama wote.