1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Sharif afanya mazungumzo ya kuunda serikali

12 Mei 2013

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif ameanza mazungumzo ya kuunda serikali baada ya kushinda katika uchaguzi wa bunge nchini Pakistan

https://p.dw.com/p/18WNk
Nawaz Sharif (C), leader of the Pakistan Muslim League - Nawaz (PML-N) political party, casts his vote for the general election at a polling station in Lahore May 11, 2013. A string of militant attacks cast a long shadow over Pakistan's general election on Saturday, but millions still turned out to vote in a landmark test of the troubled country's democracy. REUTERS/Mohsin Raza (PAKISTAN - Tags: POLITICS ELECTIONS TPX IMAGES OF THE DAY)
Nawaz Sharif akipiga kuraPicha: Reuters

Sharif aliangushwa kutoka madarakani katika mapinduzi mwaka1999, akafungwa na kupelekwa uhamishoni. Nawaz ameweza kurejea tena kwa kishindo na kushiriki katika uchaguzi. Nawaz Sharifi atakuwa Waziri Mkuu kwa mara ya cha tatu nchini Pakistan.

Kituo cha binafsi cha televisheni cha Geo kimeripoti kuwa chama cha Nawaz cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) kiliongoza katika majimbo 126 ya ubunge kati ya majimbo 268 .

Kituo cha televisheni cha Dunya kimesema kuwa chama cha PML-N tayari kimepata viti 80. Kituo cha taifa cha televisheni nchini Pakistan pia kimesema chama hicho kinaongoza.

Matokeo ambayo si rasmi yanaonesha kuwa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf cha aliekuwa mchezaji nyota wa kriketi Imran Khan kiko katika nafasi ya pili.

Chama tawala cha zamani cha Pakistan Peoples Party cha rais Asif Ali Zardari kinafuatia.

A Pakistani election official empties a ballot box at the end of polling in Islamabad on May 11, 2013. Polling stations closed at 6:00 pm (1300 GMT) in Pakistan's historic general elections, which saw a "huge" turnout in the largest province of Punjab, an election commission official announced. AFP PHOTO / AAMIR QURESHI (Photo credit should read AAMIR QURESHI/AFP/Getty Images)
Kura zikianza kuhesabiwaPicha: AAMIR QURESHI/AFP/Getty Images

Vyama vya kidini havikufua dafu

Vyama vya kidini vyenye mtazamo wa mrengo wa kulia vimeshindwa kupata mafanikio ya maana.

Maafisa wa uchaguzi wamesema kuwa watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni kiasi ya asilimia 60 ya wapiga kura milioni 86 wenye haki ya kupiga kura , ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kujitokeza kupiga kura. Asilimia 44 tu ya wapiga kura walijitokeza katika uchaguzi mkuu mwaka 2008.

Uchaguzi wa kihistoria

Uchaguzi huo ni wa kwanza katika historia ya nchi hiyo , ambapo kunafanyika mabadiliko kwa njia ya kidemokrasia kutoka utawala mmoja wa kiraia kwenda kwenda kwa mwingine.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Fakhruddin Ibrahim amejiita "mtu mwenye furaha", baada ya kutangaza kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa uwazi.

"Sasa mpira uko upande wenu, mtaamua kupata serikali yenye utawala mzuri," jaji huyo mstaafu ameuambia mkutano na waandishi wa habari mjini Islamabad.

Ghasia

Ghasia za siku ya uchaguzi hata hivyo zimesababisha vifo vya watu 28 na wengine 91 wamejeruhiwa katika mashambulio ya mabomu pamoja na mashambulio yaliyolenga maeneo maalum.

Supporters of the Pakistan Muslim League - Nawaz (PML-N) celebrate in front of a party office as results of the general election come in, in Lahore May 11, 2013. Former Prime Minister Nawaz Sharif said on Saturday his PML-N party was the clear winner in Pakistan's general election and that he hoped for a majority to avoid a coalition. REUTERS/Damir Sagolj (PAKISTAN - Tags: TPX IMAGES OF THE DAY ELECTIONS POLITICS)
Mashabiki wa nawaz wakifurahia kuchaguliwa kwakePicha: Reuters

Kwa jumla viti 272 vinagombaniwa katika bunge la taifa , baraza la wawakilishi ambalo lina jukumu la kuunda serikali. Katika majimbo manne ya uchaguzi , uchaguzi umefutwa kutokana na sababu za kiusalama.

Uchaguzi huo pia unajumuisha viti 577 katika mabunge manne ya majimbo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri : Amina Abubakar