1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Sharif atarajiwa kurejea Pakistan hii leo

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSgp

Waziri mkuu wa zamani wa Paksitan, Nawaz Sharif, anatarajiwa kurejea nyumbani kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia hii leo. Mpambe wa kiongozi huyo, Sadiq al Farroq, amesema Nawaz Sharif pamoja na watu wengine wa familia yake, watarejea mjini Lahore mashariki mwa Pakistan.

Tangazo la kurejea kwa Nawaz Sharif limetolewa baada ya mkutano wake na mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na kiongozi wa ujasusi Mwanamfalme Maqren bin Abdul Aziz mjini Riyadh hapo jana.

Afisa wa cheo cha juu wa serikali ya Pakistan amesema hakuna mpango wa kumkatamata Nawaz Sharif akisema kuwa rais Musharraf ameahidi kuvipa vyama vyote vya kisiasa nchini Pakistan nafasi sawa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi Januari mwakani.