1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Sharif kurudi kesho Pakistan

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRL

LONDON:

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif amesema leo ametia nia kweli kurejea kesho nyumbani Pakistan licha ya wasi wasi juu ya athari za uamuzi wake kwa utulivu wa Pakistan.

Huko Pakistan kwenyewe ulinzi mkali uliimarishwa hii leo kote nchini n a kweenye uwanja wa ndege.Chama cha nawaz sharif cha Muslim League kimearifu kuwa wanachama wake hadi 2000 wametiwa nguvuni na kuwekwa kizuizini.

Afisa mmoja wa polisi katika mkoa wa Punjab –shina la Nawaz Sharif ,amesema wamewaweka kizuizini wafanya fujo 250.