1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakopeshaji ni majaji

5 Julai 2015

Kushindwa kwa mazungumzo na Ugiriki kunaonyesha kutokuwepo kwa itifaki za kufilisika na kwamba bila ya kuwepo kwa mipango hiyo sakata la Ugiriki litakuwa halina mwisho anairipoti Andreas Becker wa DW.

https://p.dw.com/p/1Ft4U
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras wakati wa kupiga kura yake ya maoni.(05.07.2015)
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras wakati wa kupiga kura yake ya maoni.(05.07.2015)Picha: Reuters/C. Hartmann

Wakati kampuni au mtu binafsi anapotowa taarifa za kufiliska mchakato wa kufilisika unatakiwa uratibiwe na sheria. Kesi huwa inawakilishwa mbele ya jaji na taasisi isio na upendeleo yaasi sio mkopeshaji au wakopeshaji wanaamuwa hatua za kuchukuliwa baada ya hapo.

Hivi sivyo iliyokuwa kwa kesi ya Ugiriki.Hapa ni wakopeshaji wenyewe ndio majaji na waendesha mashtaka dhidi ya mdaiwa.Mataifa wakopeshaji yamekuwa yakitapatapa kuhami maslahi yao wakati huo huo wakiviita vitendo vyao kuwa vya uokozi katika mazungumzo yanayofanyika chini ya mazingira ya kutoaminiana na kushutumiana.

Mwanafilosofia Jürgen Habermans anona mapungufu hayo ya wanasiasa wa Ulaya yakijitokeza katika hali hiyo. Ameandika hivi karibuni katika makala ya gazeti la Ujerumani la "Südeutsche Zeitung " kwamba "wanaonekana kama wanasiasa lakini maneno wanayoyatamka yanaelekezwa moja kwa moja na dhima yao wakiwa kama wakopeshaji.

Upinzani wa mabenki

Mazumgumzo hayo yalioshindwa yameonyesha matatizo kutokana na dhima nyingi ilizokuwa nazo nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.Wakiwa wakopeshaji wanataka kumlazimisha mdaiwa kupunguza matumizi fulani ya bajeti wakati huo huo ikidhibiti utekelezaji wa mapunguzo hayo.

Wagiriki wanaopinga mapendekeozo ya wakopeshaji.
Wagiriki wanaopinga mapendekeozo ya wakopeshaji.Picha: Reuters/Y. Behrakis

Kuhusishwa kwa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF shirika linaloshughulikia mahsusi nchi zilizokumbwa na madeni kunazidi kuonyesha kuwepo kwa mgongano wa maslahi wa Ulaya.

IMF ilianza kushinikiza kuwepo kwa sheria za kufilisika mapema miaka ya 2000 lakini hadi sasa juhudi zao hizo zimeshindwa kuzaa matunda.

Muasisi mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Flossbach von Strorch Thomas Mayer ameiambia DW kwamba wakati ule mabenki ya kimataifa yalipinga wazo hilo.

Katika kesi ya Ugiriki wakopeshaji pia wanatumika kama majaji.

Mabenki yalipendelea IMF iingile kati kwa kutowa mkopo mpya kwa njia mbayo wangeliweza kulipwa fedha zao zote.Mayer anaufahamu msimamo wa shirika hilo kwani aliwahi kuwa mchumi mkuu wa Deutsche Bank haid hapo mwaka 2012.

Sheria za muflisi

Pia kuna hoja nyengine dhidi ya sheria za kufilisika. Miongoni mwao ni masuala ya kisheria juu ya kwa kiasi gani uhuru wa nchi hauwezi kuingiliwa.Lakini matatizo hayo tayari yamekuwepo.Kwa mfano mwaka 2011 Ujerumani,Ufaransa na nchi za Ulaya zilimpiga marufuku waziri mkuu wa Ugiriki wa wakati huo George Papapendrou kuitisha kura ya maoni ya taifa juu ya hatua inayopaswa kuchukuliwa katika suala la mzozo wa madeni wa Ugiriki.

Wastaafu wakigombania kuingia benki.
Wastaafu wakigombania kuingia benki.Picha: Getty Images/AFP/A. Tzortzinis

Kufilisika kwa taifa pia kwa muda mrefu kumekuwa kukihesabiwa kuwa ni tatizo ambalo huzikumba nchi zinazoendelea tu.Kwa ajili hiyo Mayer anasema mpango wa kufilisika kwa nchi za Ulaya kamwe haukuwahi kuandaliwa na kwamba Ugiriki inaonekana kuwa ni kesi ya nadra tu kwa hiyo mpango huo ulikuwa hauhitajiki.

Kutokana na ukosefu wa sheria za kufilisika IMF hivi sasa inashinikiza fikra ya masamaha zaidi wa madeni kwa Ugiriki jambo ambalo linapingwa na nchi za Ulaya. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na wenzake ni wanasiasa wanaofahamu vya kutosha ghadhabu za wapiga kura. Ujumbe wa hamasa wa Merkel kwa Wagiriki ni kwamba deni lazima lilipwe.

Katika mahojiano na gazeti la wiki la Ujerumani la "Die Zeit " mchumi wa Ufaransa Thomas Piketty amesema "Huo ni mzaha! Ujerumani ni nchi ambayo katu haikuwahi kulipa madeni yake.Haiwezi kuzihubiria nchi nyengine katika suala la madeni."

Msamaha wa madeni

Katika makubaliano ya madeni ya mwaka 1953 mjini London wakopeshaji wengi miongoni mwao Ugiriki walisamehe sehemu kubwa ya madeni ya taifa changa wakati huo Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani na kuufanya uchumi wa kipindi cha baada ya vita kunawiri wakati huo ukijulikana kama "Wirtschaftswunder" yaani miujiza ya kuchumi.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na waziri wake wa fedha Wolfgang Schaeuble.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na waziri wake wa fedha Wolfgang Schaeuble.Picha: Reuters

Kwa mujibu wa Johannes Mayr mchumi mwandamizi katika benki ya BayerrnLB mojawapo ya mabenki makubwa nchini Ujerumani kwa njia moja au nyengine kutakuwepo na punguzo jengine la madeni licha kupingwa na Ujerumani na nchi nyengine za Ulaya.

Ameiambia DW jambo hilo litafanyika wazi wazi au yumkini zaidi kwa ufumbuzi wa tatizo hilo unaweza kuahirishwa uje kushughulikiwa baadae.

Sheria za kufilisika na msamaha wa madeni vimebuniwa ili kuzuwiya athari kubwa na wakati huo huo kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa mzozo wa madeni.

Mwandishi :Andreas Becker/ Mohamed Dahman/DW

Mhariri : Yusra Buwayhid