1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika kufikiria kuwekeza katika mipango ya mazingira

Saumu Mwasimba
21 Machi 2023

Nchi za kiafrika kufikiria kubadilishana madeni yake na mipango ya uwekezaji katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira.

https://p.dw.com/p/4OzRg
Äthiopien | AU Gipfel in Addis Ababa
Picha: Solomon Muchie/DW

Uamuzi wa nchi hizo masikini ambazo pia zinazongwa na madeni na hasara iliyosababishwa na uharibifu kutokana na matukio ya vimbunga, ukame na joto kali zimekubaliana hilo katika mkutano wa mawaziri wa fedha uliofanyika Addis Ababa siku ya Jumatatu.

Hatua hiyo itazifanya  nchi masikini kupunguziwa madeni yake  na badala yake nchi hizo za Afrika  zitahitajika kuahidi kuwekeza katika mazingira.

Waziri wa fedha wa Misri Mohammed Maait amesema kwamba nchi yake ni moja kati ya nchi nyingi ambazo hivi sasa  zinalazimika kuongeza fedha nyingi katika bajeti yake ya mazingira ambayo imepunguwa kwa kiasi kikubwa kutokana na madeni ya nje.