1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Afrika zashirikiana dhidi ya Umoja wa Ulaya

Ramadhan Ali30 Agosti 2007

Nchi nyingi za Afrika zina wasi wasi wa kuzifungulia wazi milango ya masoko yao nchi za Ulaya chini ya mapatano mapya yanayochukua nafasi ya yale ya Lome.

https://p.dw.com/p/CH8n
Biashara ya bidhaa za kilimo ni suala moja linalozusha mjadala kati ya Ulaya na Afrika
Biashara ya bidhaa za kilimo ni suala moja linalozusha mjadala kati ya Ulaya na AfrikaPicha: AP

Zikiingiwa na wasi wasi kwamba yatajipatia kidogo kwa kuridhia mengi,nchi nyingi za kiafrika kupinga baadhi ya mashauri yaliopendekezwa ili kuwa na uhusiano mpya wa kibiashara na Umoja wa Ulaya mwaka ujao.

Nchi nyingi za Afrika mashariki na kusini mwa Afrika zimetangaza kwamba ziko tayari tu kutia saini sehemu tu ya mapatano ya ushirikiano wa kiuchumi na Umoja wa ulaya maarufu kwa jina la (EPAS).

Ni mapatano haya yanayohusiana na kumfungulia mwenzake soko pamoja na misaada ya maendeleo.Mapatano ya EPA yamekusudiwa kuchukua nafasi ya yale COTONOU yanayomalizika muda wake mwishoni mwa desemba mwaka huu.

Mapatano ya Cotonou yanazipa nchi 77 za Afrika,Caribbean na Pacific au nchi za (ACP) nafasi ya kuingiza bidhaa zao kwa bei nafuu katika masoko ya Umoja wa ulaya .Yakiwa yametiwa saini huko Benin, hapo juni,2000,mapatano haya yashika nafasi ya yale ya Lome, yaliofungwa nchini Togo, miaka 25 iliopita.

Wakati wa mkutano wa mashariki na kusini mwa Afrika, huko Port Louis,Mauritius,hapo August 3-5, nchi 16 za COMESA ,ziliafikiana mkakati wa kuufikisha katika duru ijayo ya majadiliano itakayofanyika mwezi ujao wa septemba.

Nchi 16 za COMESA,hazina njia nyengine bali kutia saini vifungu vya mapatano hayo mapya ili kubakisha nafuu zao za kibiashara zinazopata katika soko la Umoja wa ulaya na kubakia zina sauti katika shirika la Biashara Suniani (WTO).

Wakati huu nchi za ACP zinafaidika na fursa maalumu za kibiashara kutoka Umoja wa ulaya ambazo hazibidi nazo kutoa kwa Umoja huo-fursa ambazo hazilingani na masharti ya Shirika la Biashara duniani (WTO).

Kwahivyo, masharti mapya ya kibiashara yanazunguzmzwa sasa kupitia kuanzishwa mapatano ya EPA yanayotarajiwa kuanza kazi hadi mwisho wa mwaka huu 2007.Lakini, mazungumzo ya EPA yamebainika kupambana na shida huku baadhi ya nchi zikihofia uchumi wao hautaweza kukabili mashindano makali ya bidhaa kutoka ulaya zitzakazoingia masoko yao.

Katika mkutano uliofanyika mjini Brussels, hapo Februari, wajumbe wa COMESA walisema hasara kubwa kwa mapato ya nchi nyingi za kiafrika zinazotegemea mno ushuru wa forodha, kutaulazimisha Umoja wa Ulaya, kuzifidia nchi hizo kwa kima cha Euro bilioni 2 zaidi ifikapo 2010- ikiwa wafungue masoko yao kwa bidhaa za ulaya.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukituhumiwa na wachambuzi wa sera za vyakula na biashara katika nchi changa, kwamba hazivumilii bidhaa za aina hiyo kuingia bila vikwazo katika masoko yao.Na hii nchi changa zinaona, ni ujanja wa kulinda masoko yao yasiingiliwe.

Kosa jengine ambalo baadhi ya wachunguzi barani Afrika wanalinyoshea kidole: ni ule mfano wa Umoja wa Ulya kuitumia Afrika kusini kama kipimo cha uwezo wa bara zima la Afrika,katika kujikinga na hasara za mapato zinazoweza kutokana na mapatano ya EPAS.

Afrika kusini yenye maliasili nyingi na ilioendelea kibiashara mawasiliano na kwa miundo-mbinu, ina pato la kila mkaazi la dala 13,300 kwa mwaka uliopita nah ii licha ya ukosefu wa kazi wa kima cha kiasi 25%.

Msumbiji,jirani yake, pato lake kwa kila mkaazi la dala 1,500 ,Kenya dala 1.200 na Tanzania dala 800, ziko nyuma kabisa ya Afrika kusini.Kwahivyo, si sawa kuzitia zote chungu kimoja.