1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za kiafrika zinapania kuimarisha usalama wa safari za ndege

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2p

Addis Ababa:

Mawaziri wa usafiri wa nchi za Umoja wa Afrika waliokua wakikutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia,wameidhinisha “taarifa ya pamoja kuhusu usalama wa safari za ndege barani Afrika”.Taarifa hiyo imetangazwa mnamo siku ya mwishoni ya mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu safari za ndege barani Afrika.Taarifa hiyo imelengwa kuimarisha mapambano dhidi ya “shughuli za usafiri ambazo ni kinyume na sheria”.”Mataifa yanabidi yajitahidi zaidi katika kupiga vita safari za ndege na shughuli za kusafirisha bidhaa kinyume na sheria) na kuimarisha usalama wa angani” amesema mwenyekiti wa mkutano huo , waziri wa usafiri wa Kongo Brazaville Emile Ouosso.Kwa maoni yake nchi za kiafrika zinabidi zipambane na matatizo ya kila aina ikiwa ni pamoja na kuboresha shughuli za kiufundi katika viwanja vya ndege ,kuepusha kitisho cha kukimbiwa na wataalam wa kiafrika ,na kuzidi kuwatanabahisha jamii juu ya umuhimu wa usalama katika viwanja vya ndege.Mkutano huo umeitishwa katika wakati ambapo ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways imeanguka mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Douala Cameroun na kugharimu maisha ya watu 114.