1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za OPEC zimeamua kutozidisha mafuta

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXYP

Nchi wanachama 13 wa OPEC-shirika la nchi zinazozalisha mafuta zimeamua kutozidisha uzalishaji wa mafuta kusaidia kushusha bei ya mafuta katika masoko ya dunia.Shirika hilo limeshinikizwa na wanunuzi kuongeza mafuta,baada ya bei ya pipa moja la mafuta ghafi hivi karibuni kuvunja rekodi na kufika hadi Dola 99.

Mawaziri wa nchi wanachama wa OPEC wamekutana Abu Dhabi,mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu kujadili suala hilo.Nchi za OPEC huzalisha asilimia 40 ya mahitaji ya mafuta duniani. Shirika hilo litakutana tena mwezi wa Januari kujadili viwango vya uzalishaji wa mafuta.