1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya Iran Air yaanguka milimani

P.Martin/ZPR10 Januari 2011

Hadi watu 70 wameuawa na wengine 35 wamejeruhiwa katika ajali ya ndege iliyotokea katika hali mbaya ya hali ya hewa, kaskazini-magharibi ya Iran.

https://p.dw.com/p/QpI5

Ndege hiyo ya Boeing 727 ya shirika la ndege la serikali Iran Air,ilianguka ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa mji wa Urumiyeh ulio katika eneo la milimani. Wakati wa ajali hiyo kulikuwepo dhoruba kali ya theluji na ukungu mzito. Ripoti zinasema kuwa rubani wa ndege hiyo, hapo awali aliripoti kuhusu tatizo la kiufundi.Ndege hiyo ilitokea mji mkuu wa Iran, Teheran.

Mwandiashi:Prema Martin/ZPR

Mpitiiaji:Hamidou Oummilkheir