1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege za Israel zaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza

P.Martin3 Januari 2009

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon sawa na Rais wa Marekani George W.Bush ametoa mwito wa kusimamia usitishaji wa mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas katika Gaza.

https://p.dw.com/p/GRHG
Smoke is seen from explosions after an Israeli airstrike in the outskirts of Gaza City, Friday, Jan. 2, 2009. Israel showed no sign of slowing a blistering seven-day offensive against Gaza's Hamas rulers, destroying homes of more than a dozen of the group's operatives Friday and bombing one of its mosques a day after a deadly strike killed a prominent Hamas figure. (AP Photo/Adel Hana)
Miripuko iliyosababishwa katika mashambulizi ya anga ya Israel ukingoni mwa mji wa Gaza.Picha: AP

Rais Bush ameilaumu Hamas kwa hali iliyozuka hivi sasa kwenye Ukanda wa Gaza.Amesisitiza kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano hayawezi kupatikana mpaka Hamas itakapoacha kurusha maroketi dhidi ya Israel.

Hapo awali,mratibu mkuu wa misaada ya Umoja wa Mataifa kwa eneo hilo,Maxwell Gaylard alisema, maafa ya kibinadamu yanachomoza katika kanda hiyo,kwa sababu misaada ya chakula,dawa na mahitaji mengine imezuiliwa.Israel inashikilia kuwa bado kuna chakula na dawa za kutosha katika eneo la Gaza, licha ya operesheni yake ya kijeshi iliyoanzishwa kujibu mashambulizi ya roketi ya Hamas.Kwa mujibu wa maafisa wa Kipalestina,zaidi ya watu 420 wameuawa na wengine 2,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel ya siku saba mfululizo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech,Ufaransa na Sweden wanatazamia kwenda Mashariki ya Kati siku ya Jumapili,huku zikiwepo ishara kuwa vikosi vya nchi kavu vya Israel vimekaa tayari kuvamia Ukanda wa Gaza.