1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NDJAMENA: Chad yatangaza hali ya hatari maeneo ya mapigano

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FK

Serikali ya Chad imetangaza hali ya hatari katika mashariki ya nchi,mpakani na jimbo la Sudan la Darfur na kaskazini mwa nchi ambako makundi hasimu ya kikabila yalipambana hivi karibuni. Taarifa ya serikali imesema,hali ya hatari itabakishwa kwa kipindi cha siku 12 ili kuwapa wanajeshi muda wa kuwasaka waasi na kuwanyanganya silaha.Hadi watu 20 wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni nchini Chad.