1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NDJAMENA : Rais Deby akubali kikosi cha Umoja wa Ulaya

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgx

Rais Idriss Deby wa Chad amesema anaunga mkono kimsingi wazo la kuwekwa kwa kikosi cha muda cha Umoja wa Ulaya nchini mwake.

Kikosi hicho kinatazamiwa kuwalinda watu walioathirika na umwagaji damu ambao umesambaa kutoka jimbo la Dafur la nchi jirani ya Sudan.Deby alitowa kauli yake hiyo baada ya kukutana na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa ambaye alipendekeza kikosi hicho.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya wiki ijayo wanatarajiwa kuanza kupanga shughuli za kulinda amani zitakazowezwa kufanywa na kikosi hicho kwa kati ya miezi sita hadi 12 nchini Chad.

Umoja wa Mataifa unasema mashariki mwa Chad kuna wakimbizi takriban 230,000 kutoka Sudan na kwamba zaidi ya wakimbizi 170,000 raia wake wenyewe wamepotezewa makaazi yao kutokana na mzozo huo wa Dafur.