1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’DJAMENA : Waanza kuhojiwa kwa kutorosha watoto

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AG

Mahakimu nchini Chad leo wameanza kuwahoji kundi la wazungu 16 wanaokabiliwa na mashtaka ya utekaji nyara na hujuma kwa njama ya kuwatorosha watoto 103 kutoka nchi hiyo.

Wazungu hao wamefikishwa kwenye mahkama kuu mjini N’djamena chini ya ulinzi mkali.

Wafaransa tisa na Wahispania saba walikamatwa kwenye mji wa mashariki wa Abeche ulioko mpakani na jimbo la Dafur la Sudan zaidi ya wiki moja iliopita wakati wakijaribu kuwasafirisiha watoto hao wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi 10 kwenda Ulaya.