1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NDJAMENA: Wanajeshi wananane wauwawa

10 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCB1

Serikali ya Chad imesema wanajeshi wanane waliuwawa wakati walipokuwa wakizima shambulio la kundi la waasi kutoka nchi jirani ya Sudan.

Katika mapambano hayo, waasi kadhaa waliokuwa katika msafara wa magari 200 pia waliuwawa.

Wiki iliyopita vikosi vya Chad viliyashambulia kwa mabomu maeneo ya waasi mashariki mwa nchi hiyo, ambako machafuko yamezuka tena baada ya kipindi cha utulivu tangu mwezi Februari mwaka huu.