1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’DJAMENA : Wazungu 7 wa mzozo wa watoto waachiliwa

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79p

Raia saba wa Ulaya waliokamatwa nchini Chad kwa madai ya kujaribu kuwateka nyara watoto wamerudi nyumbani.

Waandishi habari watatu wa Ufaransa na wahudumu wa ndege wanne wa Uhispania waliondoka kutoka Chad hapo jana kwa ndege ya Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa.

Sarkozy alifanya ziara fupi kwa nchi hiyo ya Afrika kujadili kesi hiyo.

Wazungu 16 na raia kadhaa wa Chad walikamatwa kwa kujaribu kuwatorosha watoto 103 wa Afrika kuwapeleka barani Ulaya wiki mbili zilizopita.

Watu sita kati ya tisa ambao wanaendelea kushikiliwa nchini Chad ni wanachama wa shirika la misaada la Zoe Ark ambalo limesema watoto hao walikuwa ni mayatima kutoka jimbo la Sudan lililoathiriwa na vita la Dafur.

Mashirika ya misaada ya kimataifa yamesema kwamba wengi wa watoto hao walikuwa sio mayatima na hawatokei Sudan.

Jambo hilo lote limefanyika kwa sababu za kibinafsi.Mtu mmoja analishikilia mateka taifa zima kwa maslahi yake.Alikuwa anataka kuwa rais kwa kipindi kengine na pengine hukumu dhidi yake ilikuwa inakuja kutoka Mahkama Kuu ya Pakistan na ameizima hatua hiyo kwa kuchukuwa hatua hii kali dhidi ya Mahkama Kuu na bila ya shaka jamii nzima ya kiraia ya nchi hiyo.