1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’djamena.Baada ya mapigano kila upande unadai umeshinda.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxg

Baada ya kutokea tena kwa mapigano makali nchini Chad, pande zote mbili za majeshi ya Rais Idriss Deby na upande wa waasi zimedai kuibuka mshindi, lakini waangalizi nchini humo wamesema kuwa majeshi ya serikali yamepata hasara kubwa zaidi.

Waziri wa Ulinzi Bichara Issa Djadallah amesema, jeshi limewauwa kiasi ya waasi mia moja na limepoteza wanajeshi wanne tu kufuatia mapigano ya hapo jana karibu na mpaka wa Sudan.

Vile vile amekiri kumpoteza Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi katika mapigano hayo.

Hata hivyo waasi waliokuwa mtari wa mbele katika mapigano wamedai wamewauwa wanajeshi wa serikali 215 na wao wamepoteza wapiganaji wao 15.

Taarifa ya serikali imesema kuwa, Naibu Mnadhimu Mkuu wa jeshi, Jenerali Moussa Sougui ameuwawa katika mapigano.

Kufariki kwa Jenerali Moussa kumetajwa kuwa ni pigo kubwa kwa taifa na kinachokumbusha kifo cha Jenerali Abakar Yousouf Itno ambae alikuwa ni kamanda wa jeshi na mjomba wake rais Deby kilichotokea mwezi March.