1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NDJAMENA:Mapambano yazuka baina ya waasi na majeshi ya Sudan

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4f

Majeshi ya Sudan yamepambana na waasi wa Darfur kwenye mpaka baina ya Sudan na Chad.

Waasi hao wanapinga makubaliano yaliyotiwa saini hivi karibuni juu ya kuleta amani katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.

Pande hizo mbili zimelaumiana kwa kuanzisha mapigano hayo.Habari zinasema watu zaidi ya 70 walijeruhiwa .

Msemaji wa waasi hao amedai kuwa wapiganaji wao wamewateka askari 100 wa Sudan, ikiwa pamoja na Brigedia.

Wakimbizi wa Sudan zaidi ya laki mbili wanaishi kwenye kambi zilizopo karibu na mpaka baina ya Sudan na Chad.