1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’djamena.Watu 220 wauwawa huko Chad wiki hii.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuG

Watu wenye silaha wakiwa wamepanda farasi, wamewauwa kiasi ya wanakijiji 220, mashariki mwa Chad katika wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, kiasi ya vijiji saba vilishambuliwa karibu na mpaka wa kusini mwa Sudan.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia wakimbizi, Antonio Guterres amesema hapo jana kuwa, shirika lake limeonya kwa karibu mwezi mmoja sasa, kwamba mgogoro wa Darfur ni tishio kwa nchi nyengine zilizo karibu na jimbo hilo la Sudan.