1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aimarisha nafasi ya kuwa waziri mkuu mpya Israel

Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP19 Februari 2009

Benjamin Netanyahu aungwa mkono na chama cha Yiesrael Beiteinu

https://p.dw.com/p/GxYr
Kiongozi wa upinzani nchini Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Kiongozi wa upinzani nchini Israel Benjamin Netanyahu ameimarisha nafasi yake ya kuwa waziri mkuu mpya wa Israel baada, ya kupata uungaji mkono wenye masharti kutoka chama cha Yisrael Beiteinu. Kiongozi wa chama hicho Avigdor Lieberman amemtaka Netanyahu kuunda serikali itakayo vijumuisha vyama vikuu vya kisiasa nchini humo



Netanyahu na kiongozi wa chama cha Kadima Tzipi Livni walijitangaza washindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 10 mwezi huu nchini Israel. Matokeo rasmi yalikipa Chama cha Kadima ushindi wa viti 28 kati ya viti 120 vya bunge na Likud kujipatia viti 27.


Rais Shimon Perez wa Israel ameanza mazungumzo ya kumchagua kiongozi atakaekabidhiwa wadhifa wa waziri mkuu. Baada ya kuzungumza na kiongozi wa chama cha Yisrael Beiteinu, Avigor Liebermann amependekeza Netanyahu akabidhiwe wadhifa huo na kusema

"Hali namna ilivyo hapa nchini inalazimisha pawepo serikalio madhubuti,haraka iwezekanavyo.Tunamuunga mkono Benjamin Netanyahu,linapohusika suala la kuunda serikali ya muungano ya vyama vingi.Ili kuweza kutia njiani utaratibu wa kisiasa,panahitajika serikali ya vyama vitatu vikuu vya kisiasa-Likud,Kadima na Yisrael Beiteinu.Anaetaka kujiunga nasi baadae,anaweza..."


Chama cha Yisreal Beiteinu cha Bw Liebermann kimegeuka kua nguvu ya tatu ya kisiasa nchini Israel kwa kujikingia viti 15 katika uchaguzi uliopita wa bunge.


Kiongozi huyo wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia,mashuhuri kwa matamshi yake makali dhidi ya waisrael wenye asili ya kiarabu,amemtaka kiongozi wa Likud,Benjamin Netanyahau azingatie upya msimamo wake na kusema:

"Ndio maana tunawaeleza marafiki zetu wa Likud,Anzeni kufikiria upya.Hii itakuwa serikali ya Netanyahu na Livni.Watu hao wawili watabidi wabuni mkakati wa pamoja na kukubaliana mwongozo wa iana moja.Na kama nilivyosema Netanyahu atabidi atambuwe tunazungumzia kuhusu muungano wa vyama vingi na sio kinyume chake,na Zippi Livni atabidi atambue kuwa hakutakuwa na kubadilishana zamu"


Rais Shimon Perez anatazamiwa kumaliza mashauriano yake na viongozi wa vyama vya kisiasa kesho na kupitisha uamuzi haraka juu wa nani aunde serikali ya muungano.


Hapo jana Rais Perez alikutana na wachama kutoka chama cha Kadima, na hivi leo alipangiwa kukutana na wawakilishi kutoka vyama vingine 10 vya kisiasa nchini humo vyenye uakilishi bungeni.


Chini ya katiba ya Israel anayepewa jukumu la kuunda serikali anapaswa kukamilisha kibarua hicho katika muda wa siku 42.

Peres ana hadi tarehe 25 mwezi huu kumtangaza aliyeamua kumpa jukumu hilo.