1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu akubali kupeleka wajumbe wa Israel Misri na Qatar

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akubali kupeleka wajumbe wa Israel Misri na Qatar kuendeleza mazungumzo ya kuachiwa huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

https://p.dw.com/p/4eG8s
Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kwa ajili ya sitishaji mapigano Gaza
Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kwa ajili ya sitishaji mapigano GazaPicha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekubali kutuma ujumbe wa Israel nchini Misri na Qatar, ambako wapatanishi wamekuwa wakitafuta mbinu za kuachiwa huru watu waliochukuliwa mateka na Hamas, kama sehemu ya makubaliano yanayotafutwa ya kusitisha mapigano kwa muda ili misaada zaidi pia iweze kufikishwa Gaza.

Ofisi ya Netanyahu imesema Waziri Mkuu huyo alizungumza na wakuu wa taasisi ya usalama ya Israel Shin Bet na kiongozi wa shirika la ujasusi la Israel Mossad na kuidhinisha ujumbe wa Israel, kuondoka katika siku kadhaa zijazo kuelekea Doha na Cairo ili kuendeleza mazungumzo hayo.

Wapatanishi kutoka Marekani, Misri na Qatar wamejaribu kupata suluhu ya mgogoro unaoendelea Gaza lakini mazungumzo yaliyoanzishwa yanaonekana kukwama ikiwa ni takriban siku ishirini baada ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhan uliyo muhimu kwa waumini wa kiislamu.