1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu anataka kukutana ana kwa ana na Abbas

Martin,Prema/zpr20 Septemba 2011

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu angependa kukutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas, pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

https://p.dw.com/p/Rmhu
Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu chairs the weekly cabinet meeting at his Jerusalem office on 05 September 2010. Prime Minister Benjamin Netanyahu's media advisor Nir Hefetz denied reports alleging Netanyahu suggested forming 12 negotiating teams and was refused by the Palestinians. 'Nothing of the kind has been suggested. On the contrary - Prime Minister Netanyahu offer the Palestinians to hold accelerated talks, once every two weeks, and in between, to have smaller, discreet meetings in order to seriously and responsibly pursue a peace agreement,' Hefetz said in a statement. EPA/MENAHEM KAHANA / POOL +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: picture alliance / dpa

Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel. Netanyahu anatoa mwito kwa serikali ya Wapalestina kurejea katika majadiliano ya ana kwa ana kutafuta suluhisho la amani. Hapo awali, Waziri Mkuu Netanyahu, aliwaonya Wapalestina kuwa amani haiwezi kupatikana kwa kuchukua hatua ya upande mmoja katika Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo, Rais wa Wapalestina Abbas amesisitiza dhamira yake ya kuwasilisha ombi la uanachama kamili, katika Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.Tangazo hilo limezusha wasiwasi katika jumuiya ya kimataifa. Waziri wa Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amezihimiza pande zote mbili kurejea katika meza ya majadiliano.

epa02717258 Palestinian President Mahmoud Abbas talks during the ceremony of reaching agreement between Fatah and Hamas in Cairo, Egypt, 04 May 2011. Palestinian President Mahmoud Abbas, leader of the Fatah party, and Hamas leader Khaled Mashaal shook hands in Cairo, Egypt on a reconciliation deal which ended a bitter four-year-long dispute between the two largest Palestinian factions. EPA/KHALED ELFIQI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Wapalestina, Mahmoud AbbasPicha: picture alliance/dpa