1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neu Ulm Ujerumani. El Masri akamatwa kwa kutuhumiwa kuchoma moto duka!

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0y

Aliekuwa mahabusu kwenye jela ya Marekani ya Guantanamo amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma moto duka moja katika mji wa Neu Ulm kusini mwa Ujerumani.

Mtuhumiwa huyo bwana Khaled el Masri aliwekwa rumande katika duka hilo, na polisi imesema kuwa baadae alipelekwa kwa daktari wa akili ili kufanyiwa uchunguzi.

Bwana el Masri aliefungwa katika jela ya Guantanamo alidai kuwa alitekwa nyara na maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani CIA nchini Macedonia na kupelekwa Afghanistan na baadae Guantanamo.