1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Kasuri asema juhudi za kutafuta amani zatakiwa kuendelea

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ5

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Pakistan, Khursid Mahmud Kasuri, amesema juhudi ya kutafuta amani kati ya nchi yake na India zinatakiwa kuendelea licha ya shambulio la bomu dhidi ya treni ya abiria.

Kasuri aliwatembelea manusura wa shambulio hilo nchini India hapo jana. Aidha Kasuri, amesema serikali mjini New Delhi na Islamabad zinahitaji kushirikiana vyema zaidi kumaliza mashambulio kama shambulio hilo dhidi ya treni lililowaua watu takriban 66.

Kasuri aliwasili nchini India jana kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo kuhusu njia za kuziendeleza juhudi za kutafuta amani baina ya India na Pakistan.

Hapo awali polisi India walimhoji mwanamume mmoja raia wa Pakistan kwa kusababisha milipuko na moto ndani ya treni hiyo ya abiria iliyokuwa njiani kwenda Pakistan ikitokea mjini New Delhi India.

Polisi pia walitoa michoro ya nyuso mbili za wanaume wanaoaminiwa waliruka nje ya treni hiyo kabla milipuko hiyo kutokea.