1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Mwito kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na India

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BR

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,hii leo anafanya ziara yake ya kwanza nchini India tangu kushika madaraka.Kabla ya kuondoka,alitoa mwito kwa sekta ya kiuchumi kujiimarisha zaidi nchini India.

Kansela Merkel amefuatana na ujumbe mkubwa wa mameneja wa makampuni makuu ya Ujerumani, wanasayansi na maafisa wa mashirika ya misaada.

Wakati wa ziara hiyo,Ujerumani na India zitatia saini makubaliano ya kushirikiana katika sekta za ulinzi,sayansi,teknolojia na haki miliki.

Mada nyingine muhimu itakayojadiliwa na Merkel wakati wa ziara yake nchini India ni mabadiliko ya hali ya hewa duniani.