1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi.Hu Jintao ahimizi ushirikiano wa kibiashara na India.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq3

Akikamilisha ziara yake ya siku nne nchini India, Rais wa China Hu Jintao amesema, nchi mbili hizo lazima zifanye kila linalowezekana ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara.

Akizungumza na viongozi shirika huko Mumbai, Hu Jintao ameelezea matumaini yake kwamba Bara la Asia litatawala katika karne hii lakini endapo China na India zitashirikiana kibiashara.

Uhusiano wa nchi mbili hizo zenye watu wengi zaidi duniani, umekuwa ukilega lega tangu wakati wa vita vya mpakani vya mwaka 1962.

Ziara ya Hu nchini India inakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Watibet, ambapo muandamanaji mmoja wa Kitibet alijitia moto nnje ya Hoteli aliyofikia Hu, huko Mumbai lakini Polisi walifanikiwa kuuzima moto huo.

Safari nyengine Hu Jintao itampeleka hadi nchini Pakistan.