1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi.Viongozi wa kidini nchini India watofautiana kuhusu hukumu ya Saddam.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvW

Viongozi wa kiislamu nchini India wamegawanyika juu ya mtazamo wa hukumu ya kifo aliyopewa Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Husein.

Viongozi wakuu wa Kisunni wanailalamikia hukumu hiyo kuwa imetolewa na mahakama walioiita ni “Mahakama ya Vibaraka” na baadhi ya viongozi wa Kishia wamesema kuwa Saddam Husssein anastahiki hukumu hiyo.

Imam wa Kisunni, Sayed Ahmed Bukhari ambae ndie kiongozi wa msikiti mkubwa nchini India unaojulikana kama Jama Masjid uliopo mjini New Delhi , aliongoza maandamano akipinga hukumu hiyo na kusema kuwa Rais wa Marekani George W. Bush ndie anaestahiki hukumu kama hiyo.

Katika maelezo yake Imam Sayed Ahmed alisema Rais Bush lazima afikishwe mahakamani kwa mauaji yake aliyoyafanya nchini Iraq ambako watu zaidi ya laki saba wameuwawa tangu Marekani ilipoivamia nchi hiyo.

Waandamanaji walionekana sehemu za Ludhiana kaskazini mwa mji wa Punjab, sehemu ambako Wasunni walizichoma moto picha za Rais Bush.