1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Azimio lataka kukomeshwa umwagaji damu

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCre

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye kutaka kukomeshwa mara moja kwa vitendo vyote vya matumizi ya nguvu vinavyofanywa na Israel na Wapalestina.

Zaidi ya nchi 150 zimepiga kura kuliunga mkono azimio hilo ambalo halishurutishi lililopendekezwa na Qatar kwa niaba ya nchi za Kiarabu.Nchi saba zikiwemo Marekani na Israel zimepiga kura kulipinga azimio hilo wakati nchi nyengine sita ikiwemo Canada hazikupiga kura.

Azimio hilo pia limamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuunda tume ya kutafuta ukweli kuchunguza mashambulizi ya Israel ya wiki iliopita katika mji wa Bet Hanun kwenye Ukanda wa Gaza ambapo watu 18 wameuwawa wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.