1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban Ki Moon apendekeza kikosi kwa ajili ya Chad na Afrika ya Kati

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYR

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametoa mwito baraza la usalama la umoja huo liidhinishe kikosi cha pamoja kitakachojumulisha majeshi ya Umoja wa Ulaya na polisi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika ripoti yake iliyowasilishwa kwa baraza la usalama, Ban Ki Moon, amesema tume anayoipendekeza itasaidia kuwalinda maelfu ya raia ambao maisha yao yamo hatarini kufuatia mzozo wa Darfur.

Mwezi Februari mwaka huu kiongozi huyo alipendekeza kikosi cha Umoja wa Mataifa kipelekwe katika eneo hilo lakini pendekezo hilo likapingwa na rais wa Chad, Idris Deby.

Rais Deby amesema atakubali kikosi kitakachokuwa na wanajeshi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya.

Mzozo wa Darfur umeenea katika nchi jirani ya Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati hivyo kusababisha tatizo kubwa la wakimbizi.