1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Ban Ki-Moon katibu mkuu mpya wa umoja wa mataifa.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD34

Baraza kuu la umoja wa mataifa lenye mataifa wanachama 192 limemuidhinisha rasmi waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya kusini Ban Ki-Moon kuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Ban anachukua nafasi ya Kofi Annan atakapoacha madaraka Desemba mwaka huu baada ya kutumikia wadhifa huo kwa muda wa miaka kumi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 62, ambaye ni mwanadiplomasia amesema kuwa anataka kutumia hali ya upole wa watu wa bara la asia kuweza kuiongoza taasisi hiyo ya dunia , lakini ameonya kuwa hali hiyo isichukuliwe kuwa ni udhaifu.

Upole unahusiana na utu, sio kuhusu mwelekeo na malengo, Ban amesema.

Atakuwa katibu mkuu wa nane tangu kuundwa kwa umoja wa mataifa mwaka 1945 na ni wa pili kutoka katika bara la Asia kushika wadhifa huo.