1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Ban Ki –Moon : Uamuzi wa kuwaruhusu wanajeshi wa UN , ishara muhimu kwa Sudan.

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9M

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ameueleza uamuzi wa Sudan wa kuwaruhusu wanajeshi 3,000 wa umoja wa mataifa kuingia katika jimbo la Darfur kama ishara muhimu.

Ujumbe huo wa umoja wa mataifa utatoa msaada kwa wanajeshi 7,000 wa umoja wa Afrika katika jimbo hilo.

Kubadilika kwa Sudan kunakuja baada ya miezi kadha ya mbinyo wa kimataifa wa kuwakubali wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani.

Lakini serikali ya Sudan haijakubali bado kuwekwa kwa jeshi kubwa zaidi la umoja wa Afrika lenye wanajeshi 20,000 ambao wamependekezwa na umoja wa mataifa.

Zaidi ya watu 200,000 wameuwawa katika jimbo la Darfur na zaidi ya milioni mbili wamekimbia makaazi yao tangu mzozo huo uanze mwaka 2003.