1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama lafikia uamuzi wa pamoja kuionya Korea Kaskazini

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5b

Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamefikia uamuzi wa taarifa ya pamoja kuionya Korea Kaskazini juu ya athari itakazokabiliana nazo iwapo itafanya jaribio la kinyuklia.

Balozi wa Japan katika baraza hilo, Kenzo Oshima, aliyeandaa taarifa hiyo, amesema nakala zitapelekwa kwa mataifa 15 wanachama wa baraza la usalama ili taarifa hiyo ifanyiwe mabadiliko kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Hata hivyo amesema taarifa hiyo inatarajiwa kuidhinishwa baadaye leo.

Wakati huo huo, maofisa wa Urusi wamesema wanawasiliana na Korea Kaskazini kujaribu kuishawishi isifanye jaribio lake la silaha ya kinyuklia.

Kuna tetesi kwamba Korea Kaskazini huenda ifanye jaribio hilo wikendi hii.