1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Bolton ajiuzulu wadhifa wa balozi.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmM

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa huo.

Tangazo hilo limekuja kabla ya Bolton , mkosoaji mkubwa wa umoja wa mataifa na mhafidhina maarufu, anakabiliwa na kikao cha kumthibitisha katika baraza la Seneti ambalo hivi sasa linadhibitiwa na chama cha Democratic, ambako inatarajiwa kuwa atakataliwa.

Rais George W. Bush amekubali kujiuzulu kwa Bolton.

Sasa anaweza kuondoka kutoka katika wadhifa huo wakati wowote kabla ya mwisho wa wiki hii.