1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK :Gordon Brown atoa wito wa kupambana na umasikini ulimwenguni

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdL

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown anatoa wito wa ushirikiano zaidi ili kupambana na umasikini ulimwenguni .Kiongozi huyo anatoa kauli hiyo baada ya kuhutubia Baraza la Umoja wa mataifa ili kuupa msukumo zaidi mpango wa ulimwengu mzima wa maendeleo uliokwama.Hatua hii inatokea baada ya mkutano wa siku mbili na Rais wa Marekani George W Bush ambapo aliunga mkono juhudi za kijeshi za Marekani nchini Iraq,Afghanistan na vita dhidi ya ugaidi.Bwana Brown alisema haya kuhusu suala la Darfur

''Hali katika eneo la Darfur ndiyo janga kubwa zaidi la kibinadamu linalokumba ulimwengu kwa sasa.Zaidi ya watu laki mbili wamepoteza maisha yao…. milioni mbili wameachwa bila makao….wengine milioni nne wanategemea msaada wa chakula. Baada ya mkutano wangu hapo jana na Rais Bush ninayemshukuru kwa uongozi wake katika suala la Darfur serekali za Uingereza na Ufaransa na mataifa mengine yanayounga mkono wameafikiana na kuandaa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha kupelekwa kikosi kilichoimarishwa cha kulinda amani na wakazi wa Darfur.''