1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Iran haitaki zaidi ya haki zake

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFb

Iran imesema haitoshinikizwa kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia wa matumizi ya amani.Siku ya Jumamosi,baada ya Iran kuwekewa vikwazo vipya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,waziri wa nje wa Iran,Manouchehr Mottaki aliliambia baraza hilo,”shinikizo na vitisho” havitobadilisha siasa ya Iran.Akaongezea kuwa Iran haitafuti ugomvi wala haitaki cho chote isipokuwa haki zake zisizoweza kuondoshwa.