1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Iran kuwekewa vikwazo vipya leo

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG1

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo litapiga kura kwa azimio la vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa kuendelea kugoma kwake kusitisha urutubishaji wa uranium.

Azimio hilo jipya linafuatia lile lililopitishwa hapo mwezi wa Desemba.Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amefuta ziara yake kwa mji wa New York ambako alikuwa alihutubie baraza hilo la usalama kabla ya mkutano wake wa kudhinisha vikwazo vipya.

Balozi wa Iran kwa Umoja wa Mataifa amesema kufutwa kwa ziara hiyo kumetokana na kuchelewa kupatiwa viza kwa ujumbe wa Ahmdedinejad.Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manochehr Mottaki atazungumza na baraza hilo badala ya rais.Maafisa wa serikali ya Marekani wamekanusha kuchelewesha utoaji huo wa viza.

Mataifa ya magharibi wanatuhumu Iran inatengeneza silaha za nuklea chini ya kisingizio cha mpango wa nuklea kwa matumizi ya kiraia dai ambalo linakanushwa na serikali ya Iran.