1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Jumuiya ya kimataifa yashutumiwa kwa kupuuzia Iraq.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGw

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limeishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kudharau maafa yanayoendelea ya kiutu nchini Iraq, ikiwa ni pamoja na kiasi watu milioni mbili ambao wamekimbia makaazi yao ndani ya nchi hiyo.

Shirika hilo la umoja wa mataifa pia linakabiliwa na mzigo mwingine wa kusaidia baadhi ya nchi kama Syria na Jordan ambazo zimewakubali wakimbizi wengine milioni mbili kutoka Iraq.

UNHCR limesema kuwa hali inaendelea kuwa mbaya kuweza kuwapatia chakula watu hao, pamoja na madawa na misaada mingine, na ikiwa kiasi cha robo ya wakimbizi hao ni watoto.