1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Jumuiya ya kimataifa yatafakari hatua dhidi ya Korea ya Kaskazini

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3z

Jumuiya ya kimataifa inatafakari hatua mujarabu za kuchukua dhidi ya Korea ya Kaskazini kufuatia hatua ya nchi hiyo kufanya jaribio la silaha za nyuklia.

Lakini China, rafiki mkubwa wa Korea ya Kaskazini , imepinga wazo la kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya nchi hiyo.Korea ya Kusini pia inapinga wazo hilo.

Hatahivyo China imesema huenda ikawa tayari kuunga mkono vikwazo vya kiuchumi .

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili mswada wa azimio uliowasilishwa na Marekani unaolenga shabaha ya kudhibiti mipango ya nyuklia ya Korea ya Kaskazini.

Marekani inataka nchi hiyo iwekewe vikwazo vya silaha, biashara na fedha.

Urusi ambayo pia inapinga wazo la kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea ya Kaskazini imetoa mwito kwa nchi hiyo irejee kwenye mazungumzo na jumuiya ya kimataifa.