1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kambi za wakimbizi zihamishwe ndani zaidi

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCo8

Chad imetoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuhamisha kambi za zaidi ya wakimbizi 200,000 kutoka eneo la machafuko la mashariki mpakani na Sudan.Katika hotuba aliyotoa kwa mabalozi wa kigeni,waziri wa masuala ya nje wa Chad amesema,kambi hizo zihamaishwe umbali wa kilomita mia kadhaa magharibi ya eneo la hivi sasa.Akaeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza madai ya serikali ya Sudan kuwa Chad inavisaidia vikosi vya waasi wa Kisudani kuwa vinatumia kambi hizo kama vituo vyake.Katika kambi hizo zinazosimamiwa na UNHCR-shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi,hasa kuna wakimbizi wa Kisudani waliokimbia mapigano katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.