1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kofi Annan amesifu misaada ya China kwa Afrika

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvy

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amefurahia tangazo la China la kuongeza maradufu msaada wake kwa bara la Afrika hadi ifikapo 2009. China ilitoa tangazo hilo kwenye mkutano wa ushirikiano wa China na Bara Afrika mjini Beijing.Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema,nchi za Kiafrika zikionyesha upya uamuzi wa kupambana na changamoto za bara hilo,sasa zinaweza kunufaika kutokana na ujuzi wa China kuendeleza uchumi na kupunguza umasikini.