1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Korea ya kaskazini yaonywa kuacha kufanya majaribio ya silaha za atomic.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5F

Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wamepiga kura kwa kauli moja kuidhinisha taarifa ya pamoja inayoitaka Korea ya kaskazini kuacha kufanya majaribio yake ya kwanza ya silaha za kinuklia.

Maafisa wa japan wanasema kuwa wanaamini Korea ya kaskazini inaweza kufanya majaribio hayo mwishoni mwa juma hili.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton , amesema kuwa nchi yake inasisitiza kupatikana mkakati maalum kutokana na kile anachokieleza kuwa ni hatua ya kuijaribu jumuiya ya kimataifa.

Korea ya kaskazini imetangaza mipango yake ya majaribio ya silaha za kinuklia wiki hii, ikisema kuwa ni muhimu kwa kuzuwia hatua za kimabavu za Marekani ,kiuchumi na kijeshi.