1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Madola makuu yafikiria vikwazo vipya dhidi ya Iran

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafikiria kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa sababu ya nchi hiyo kukataa kusitisha mradi wake wa kurutubisha madini ya Uranium.Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa,Emyr Jones Parry, aliwaarifu wanachama 10 wasio na viti vya kudumu katika Baraza la Usalama,juu ya vipengele vya azimio ambavyo vitajumuishwa na vikwazo vilivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa Desemba mwaka jana.Mswada wa azmio jipya unapendekeza kuweka vikwazo vya usafiri,silaha,fedha na biashara.Kwa mujibu wa balozi wa Ujerumani,Thomas Matussek,pendekezo la kupiga marufuku kuiuzia silaha Iran,limekabiliwa na upinzani mkali kutoka China na Urussi-nchi ambazo zina uhusiano wa karibu sana na Iran katika sekta za uchumi na nishati.