1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Majadiliano kurekebisha uhusiano wa kibalozi

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLv

Marekani na Korea ya Kaskazini kwa mara ya kwanza tangu zaidi ya miaka 50,zimeanzisha majadiliano ya kurekebisha uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.Majadiliano hayo yanafanywa kati ya makamu wa mawaziri wa nje wa nchi hizo mbili,Christopher Hill na Kim Kye-Gwan mjini New York na ni sehemu ya makubaliano yaliopatikana mwezi uliopita,baada ya Korea ya Kaskazini kukubali kuachilia mbali sehemu ya mradi wake wa nyuklia.Wadadisi wa kisiasa wanasema,majadiliano hayo ni mafanikio ya juhudi za kutaka kumaliza uhasama wa miaka na miaka,tangu Marekani katika Vita vya Korea kati ya mwaka 1950 na 1953,kuongoza vikosi vya kimataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini.