1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Majeshi ya kimataifa kutumwa Chad

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBit

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wanajadili uwezekano wa kupeleka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Ulaya nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hatua hiyo inataka kuchukuliwa kulinda wakimbizi wa Sudan wanaokimbia mapigano yanayoendelea huko Dafur kwa kukimbilia mataifa hayo jirani ya Kiafrika.Mkuu wa shughuli za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Jean-Marie Guehenno amesema iwapo hatua hiyo itaidhinishwa kikosi cha kijeshi cha Umoja wa Ulaya kitawekwa nchini Chad wakati Umoja wa Mataifa utaweka nchini humo kikosi cha polisi.

Kuna wakimbizi 230,000 wa Sudan mashariki mwa Chad na 120,000 raia wake wenyewe waliotimuliwa na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Sudan kutoka kwenye vijiji vinavyopakana na Dafur.