1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Malaria na ukimwi vinasaidiana kuleta maafa Afrika.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClO

Uchunguzi mpya wa kisayansi wa Marekani unasema kuwa magonjwa makubwa mawili katika Afrika , malaria na ukimwi , huenda yanasaidiana kusambaa katika bara hilo. Ripoti hiyo inaonesha kuwa wakati watu wenye ukimwi wanapata malaria inasababisha kuongezeka kwa virusi vya HIV katika damu, na wakati huo huo watu ambao wanadhoofika na virusi vya HIV wanauwezekano mkubwa wa kupata malaria.

Wanasayansi wanaamini kuwa mamia kwa maelfu ya maambukizo ya HIV na mamilioni ya wagonjwa wa malaria wametokana na magonjwa hayo mawili kusaidiana.